Rais wa Kenya, William Ruto, amesema hana mpango wa kufanyia Katiba marekebisho yatakayomruhusu kuendelea kuongoza taifa hilo zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano vilivyowekwa kikatiba.
Ruto amesisitiza kuwa kuheshimu mipaka ya uongozi iliyowekwa na Katiba ni muhimu kwa kudumisha demokrasia na utawala wa sheria na kwamba hatothubutu kuunga mkono juhudi zozote za kuongeza muda wa Urais.
Chanzo; Itv