Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, ameitoa onyo kali kwa Tume ya Uchaguzi, akiitaka isimamie uchaguzi kwa haki au ijiuzulu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Januari 15, 2026.
Bobi Wine ameishutumu serikali ya Rais Yoweri Museveni na chama tawala cha NRM kwa kutumia vyombo vya dola kupanga na kuhujumu mchakato wa uchaguzi. Ametahadharisha kuwa raia wa Uganda hawatakubali tena wizi wa kura, huku mvutano wa kisiasa ukizidi siku chache kabla ya uchaguzi.
Chanzo; Cnn