Waziri wa mambo ya nje wa Iran bwana Abbas Araghachi ametangaza rasmi kwamba Mlango wa Bahari wa Hormuz (Strait of Hormuz) haujafungwa kwa dunia nzima, bali umezuiwa tu kwa Marekani, Israel na washirika wao.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, meli za biashara kutoka nchi nyingine duniani zitaruhusiwa kupita kwa uhuru katika njia hiyo muhimu ya kimataifa ya usafirishaji wa mafuta.
Tamko hilo linaeleza kuwa madai ya Washington kwamba njia hiyo imefungwa kwa dunia yote hayana msingi, huku taarifa hiyo ikitangazwa hadharani kwenye matangazo ya moja kwa moja ya televisheni.
Chanzo; Global Publishers