Taarifa zinaeleza kuwa meli kubwa ya kivita ya United States imekumbwa na mlipuko uliosababisha moto mkubwa, huku zaidi ya wanajeshi 100 wakiripotiwa kujeruhiwa vibaya.
Chanzo cha tukio hilo bado hakijathibitishwa rasmi, huku vyombo vya usalama na vikosi vya uokoaji vikiendelea na juhudi za kudhibiti moto pamoja na kuwahudumia majeruhi.
Maafisa wa jeshi wameanza uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo, huku hali ya baadhi ya majeruhi ikielezwa kuwa mbaya.
Chanzo; Global Publishers