Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mtandao wa X Wapigwa Faini kwa Kukiuka Maadili

Umoja wa Ulaya (EU) umeitoza kampuni ya X, zamani ikijulikana kama Twitter, faini ya euro milioni 120 kwa kukaidi masharti ya Sheria Mpya ya Huduma za Kidijitali (Digital Services Act – DSA). Sheria hiyo inalenga kuhakikisha uwazi wa maudhui, usalama wa watumiaji na uwajibikaji katika utoaji wa taarifa kwenye majukwaa ya mtandaoni.

Kwa mujibu wa EU, mfumo wa blue checkmark wa X haukuwa na uwazi, ulikosa usawa na uliweka vikwazo kwa watafiti wanaohitaji kupata taarifa za umma kwa ajili ya tafiti za kijamii na kiusalama. Hali hiyo ilikiuka matakwa ya DSA kuhusu uwazi wa data na upatikanaji wa taarifa kwa taasisi huru za utafiti.

Hatua hiyo imefuatia uchunguzi wa miezi kadhaa ulioonesha kuwa kampuni hiyo ilificha taarifa muhimu kuhusu utambuzi wa akaunti, usimamizi wa matangazo, pamoja na namna inavyotumia mifumo yake ya kusimamia maudhui.

Tangu ununuzi wa mtandao huo na bilionea Elon Musk, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wadhibiti na makundi ya kiraia kuhusu kuongezeka kwa maudhui ya chuki, propaganda na upotoshaji wa taarifa.

EU imesema kuwa adhabu hiyo ni “hatua ya mfano” kwa kampuni zote zinazofanya biashara ya mitandao ya kijamii barani Ulaya, ikisisitiza kuwa utekelezaji wa sheria za kidijitali utasimamiwa kwa ukali ili kulinda watumiaji na kuimarisha uwajibikaji wa majukwaa makubwa ya mtandaoni.

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: