Meli ya Sun Rio imewasili katika Vladivostok, Urusi, ikiwa imebeba shehena ya magari kutoka Japani yaliyoonekana kufunikwa kabisa na matabaka mazito ya barafu.
Hali hiyo imesababishwa na baridi kali ya chini ya nyuzi sifuri pamoja na upepo mkali wa baharini uliogandisha maji juu ya magari na sehemu za meli. Tukio hilo limesababisha ongezeko la uzito wa shehena, hivyo kuhitaji uangalifu mkubwa wakati wa upakuaji ili kuepuka uharibifu wa magari na kuhakikisha usalama wa wafanyakazi bandarini.
Chanzo; Global Publishers