Alikuwa ni muuza matunda wa kawaida tu mitaani, lakini sasa Ahmed al-Ahmed, mtoto wa mkimbizi anayeishi Sydney , amegeuka kuwa shujaa wa Australia na ulimwengu kwa jumla.
Akimkabili mmoja wa washambuliaji wa Bondi Beach, alimnyang’anya bunduki na kuokoa maisha ya mamia ya wayahudi waliokuwa wakisherehekea sikukuu ya mishumaa ya Hannuka.
Pamoja na kwamba alipigwa risasi mara mbili, Ahmed anauguza majeraha baada ya upasuaji na sasa amepata umaarufu kote duniani mbali na kuchangiwa dola milioni moja na wahisani.

Chanzo; Bbc