Msemaji wa waasi wa M23, Lawrence Kanyuka, ametoa wito kwa wakazi wa mji wa kimkakati wa Uvira, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambao walikimbia kutokana na mapigano makali, kurejea katika makazi yao.
Hii inakuja baada ya M23 kuthibitisha kuuteka kikamilifu mji wa Uvira, kufuatia makabiliano makubwa kati ya wapiganaji wa kundi hilo na Jeshi la Serikali ya Kongo (FARDC), mapigano ambayo yalianza mapema mwezi huu.
Taarifa zinasema kuwa wakaazi wengi wa Uvira wamekimbilia Burundi, hasa kutokana na ukaribu wa mji huo na Bujumbura, licha ya M23 kuahidi usalama kwa wanaorejea.
Wakati huo huo, mataifa mbalimbali yakiwemo Marekani yanaendelea kusisitiza umuhimu wa utulivu na mazungumzo ya kumaliza mgogoro huo unaoendelea kutikisa eneo la Mashariki mwa Kongo.
Chanzo; Global Publishers