Kiongozi wa upinzani wa Cameroon Anicet Ekane, ambaye alimuunga mkono mpinzani mwenzake katika kinyang’anyiro cha kuwania urais dhidi ya kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Paul Biya mnamo mwezi Oktoba, amefariki akiwa kizuizini siku ya Jumatatu.
Ekane, mwenye umri wa miaka 74, kiongozi wa chama cha African Movement for New Independence and Democracy (MANIDEM), alikamatwa mnamo Oktoba 12, kufuatia maandamano ya baada ya uchaguzi katika kile ambacho chama chake kilielezea kama "utekaji nyara" wa wanajeshi wa Cameroon.
Alikuwa akishikiliwa kwa madai ya kufanya uhasama dhidi ya serikali, wito na uchochezi wa uasi, tuhuma ambazo alikanusha.
Chanzo; Dw