Mwaka wa 2011, Colin Weir na mke wake , Christine, kutoka North Ayrshire, Scotland, walishinda jackpot yenye thamani ya pauni milioni 161 zaidi ya dola milioni 200 za Kimarekani na Trilioni 5 za Kitanzani, ushindi uliowafanya kuwa miongoni mwa washindi wakubwa zaidi nchini Uingereza.

Katika miaka iliyofuata, Weir alitumia pesa zake kwa kasi ya kushangaza. Ripoti zinasema kwamba alikuwa akitumia takriban pauni 100,000 kwa wiki kununua vitu vya anasa, mali, magari, na mambo aliyopenda kama mbio za farasi na klabu yake ya soka anayoipenda sana, Partick Thistle.
Katika kipindi cha takriban miaka minane, alitumia karibu pauni milioni 40 ya zawadi yake kabla ya kifo chake mnamo 2019 kutokana na magonjwa ya figo. Ndoa yao ilivunjika muda mfupi kabla ya kifo chake.
Zaidi, Weir pia alitumia utajiri wake kwa shughuli za hisani. Alianzisha The Weir Charitable Trust, akafadhili miradi ya jamii, na akachangia pakubwa katika michezo ya ndani. Aliwekeza katika klabu ya Partick Thistle FC, na kupata hisa kubwa ambayo alikusudia kuipa wafuasi wa klabu hiyo. Pia alitoa michango mikubwa kwa misaada na sababu alizozipenda.
Wakati wa kifo chake, karibu nusu ya sehemu yake ya jackpot ilikuwa imetumika, na mali iliyobaki ya urithi wake ilipitishwa kwa watoto wake.
Chanzo; Tanzania Journal