Ripoti ya Save the Children iliyotolea Alhamisi, yasema zaidi ya watoto milioni nane wanaopaswa kuwa shuleni hawaendelei mbele na masomo yao kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Inger Ashing, Mkurugenzi Mtendajiwa Save the Children amesema kwa sasa jumuia ya kimataifa inashindwa kuwasaidia watoto wa Sudan.
Ripoti hiyo imesema kuwa zaidi ya watoto milioni nane wa Sudan wamekosa takribani siku 500 za masomo tangu vita vilipozuka Aprili, 2023.
Chanzo; Dw