Baba watoto wa mwanamuziki Rihanna, A$AP Rocky anasema wanataka kumfikia mtangazaji Nick Canon kuwa na idadi ya watoto wengi ambaye mpaka sasa ana watoto 12.
Rapa huyo A$AP Rocky ameongea hilo baada ya kuulizwa kama wana mpango wa kuongeza watoto wengine na mpenzi wake Rihanna.
"Chochote ambacho Mungu amenipa ni kama baraka! Tuna timu nzima ya mpira sasa hivi nina karibia kumfikia Nick Canon".
Mpaka sasa Rihanna na A$AP wana watoto watatu RZA Athelston Mayers aliyezaliwa 2022, Riot Rose Mayers 2023 na Rocki Irish Mayers 2023.
Chanzo; Eatv