Kanye West aliwahi kulipa takribani dola 3,900 ambayo ni sawa na Milioni 9.5 ili apate chakula alichokipenda kisafirishwe kwa ndege kutoka Wales hadi New York City.
Chakula hicho kilisafirishwa kwanza kwa helikopta, kisha kwa ndege.
Wafanyakazi wa mgahawa mmoja nchini Wales walisema oda hiyo iliomba chakula kamili cha Kihindi, ambacho walikipakia mara moja, Kilipelekwa kwa helikopta hadi uwanja wa ndege, kisha moja kwa moja kikaingia kwenye ndege na kuanza safari ya kuvuka Atlantiki.
Chakula kilifika New York siku hiyo hiyo, kikiwa bado kipo vizuri kwa Kanye na timu yake.
Mgahawa huo baadaye ulisema ilikuwa mojawapo ya oda za ajabu zaidi za watu mashuhuri walizowahi kupokea.
Chanzo; Bongo 5