Hatukufundishi wizi, lakini umewahi kushtukia mchezo huu rahisi wa kufungua kufuli bila kuvunja.
Baadhi ya kufuli hutengenezwa kwa kutumia pini zijulikanazo kama (spring-loaded). Hivyo basi kwa kutumia sumaku yenye nguvu inapowekwa juu ya kufuli, inaweza kuvuta pini hizo kwenda juu, jambo linalofanana kabisa na kazi inayofanywa na ufunguo.
Hii ndiyo sababu kufuli nyingi za kisasa zimehamia kutumia vifaa visivyoweza kuvutwa na sumaku. Ukipoteza funguo jaribu njia hii.
Chanzo; Mwananchi Scoop