Meneja wa habari na mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema Watesi wao wanahasiria za kumkosa Jonathan Sowah ndio maana wana fanya kampeni za Mshambuliaji huyo apewe adhabu za kukosa michezo ya Ligi.
Kauli hiyo imetoka mara baada ya Sowah kumfanyia madhambi Himid Mao kwa kumpiga kiwiko kwenye mchezo wa Ligi kuu ambao Mnyama Simba alipoteza kwa magoli 2-0 dhidi ya Azam Fc.
''Nguvu kubwa inatumika kumchafua na kumdhoofisha Black Lion ili kumpotezea dira yake. Watesi wetu wanatambua ubora wake na wanajua akipata muda sahihi wa kucheza atafanya mambo ya kutisha ndio maana mapambano ni makali ya kutaka kumvunja moyo. Watesi wetu wana hasira za kumkosa maana walijua kuwa timu aliyokuwepo ni mwembe wao wa uani hivyo wangemnyakua kwa urahisi kama walivyofanya kwa wengine" - Ahmed
Kwa mujibu wa kanuni ya 41:21 kuhusu udhibiti wa Wachezaji, Jonathan Sowah anaweza kukumbana na adhabu ya kufungiwa michezo mitano (5) na kupigwa faini ya milioni moja kwa kosa la kumpiga kiwiko Himid Mao.
Chanzo; Eatv