Asasi za kiraia, wadadisi wa masuala ya utawala wanasiasa na watu mbali mbali wamekosoa uhusika wa moja kwa moja wa wanajeshi katika uchaguzi nchini Uganda.
Kwa mtazamo wao mienendo hii inatishia mchakato wa kujenga demokrasia ambao msingi wake ni uchaguzi sambamba na kutishia haki za binadamu. Hii ni kutokana na utekaji unaofanywa na vikosi vya jeshi ambao umeshuhudiwa kuongezeka katika siku za hivi karibuni.
Chanzo; Dw