Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Chalamila Awataka Wanafunzi Kuacha Lama Ukosefu wa Ajira, Mawazo Njee ya Boksi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka vijana na wanafunzi nchini kufanya utafiti kabla ya kuchukua hatua zinazoongozwa na hisia, akisema kuwa kuna juhudi kubwa za kutengeneza chuki dhidi ya Serikali na viongozi wake, hasa kuelekea matukio muhimu ya kitaifa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam alipokutana na wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Chalamila amesema kuwa katika miezi ya karibuni kumekuwa na mbinu za kuwapotosha vijana kupitia mitandao ya kijamii, ikiwemo kusambazwa picha za magari yanayodaiwa kumilikiwa na watoto wa viongozi ili kuibua chuki isiyo na msingi.

Amesema mara nyingi taarifa hizo hazina ukweli na hutumiwa kuandaa mazingira ya kuamsha hasira na chuki ndani ya jamii.

Chalamila amesema chuki kama hizo hazina tija kwa taifa, na mara nyingi hutumiwa kuvuruga taswira ya serikali mbele ya wananchi wake.

Amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kuelewa madhara ya kuchoma miundombinu au kufanya vurugu, kwani vitendo hivyo huishia kuharibu rasilimali wanazozitegemea kwa maendeleo yao ya baadaye.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kutumia mifumo rasmi ya uwakilishi wa wanafunzi katika kuwasilisha hoja zao, badala ya kujiingiza katika misukumo ya kihisia.

Amesema serikali iko tayari kusikiliza na kushughulikia changamoto za wanafunzi kupitia viongozi wao wa vyuo, baraza la wanafunzi na uongozi wa kitaaluma, akisisitiza kuwa 'hasira ziende kwenye vitabu' ili kuleta hoja zenye mashiko.

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: