Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Twiga Stars ya 10 Viwango vya Ubora FIFA

Timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake Tanzania 'Twiga Stars' imepanda kwa nafasi 10 katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa mwezi Desemba.

Kwa mujibu wa viwango vilivyotangazwa juzi, Twiga Stars sasa ipo katika nafasi ya 121 kutoka ile ya 131 ambayo ilikuwepo katika chati iliyotolewa Agosti 25, mwaka huu.

Ushindi katika mechi mbili ilizocheza Oktoba za kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON) 2026 dhidi ya Ethiopia nyumbani na ugenini unaonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa kuifanya Twiga Stars kupata pointi 1,130 ambazo zimeipandisha zaidi.

Katika mchezo wa kwanza, uliochezwa Oktoba 22 hapa Dar es Salaam, Twiga Stars ilipata ushindi wa mabao 2-0 na Oktoba 28, ikapata ushindi wa bao 1-0 ugenini huko Addis Ababa, Ethiopia.

Kuwepo katika nafasi ya 121 kidunia, kunaifanya Twiga Stars kuwa kinara katika Ukanda wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ikifuatiwa na Kenya iliyo katika nafasi ya 133 na Ethiopia iliyopo katika nafasi ya 138.

Kwa Afrika, Twiga Stars inashika nafasi ya 18 huku kinara ikiwa ni Nigeria ikifuatiwa na Afrika Kusini na Ghana ambayo inashika nafasi ya tatu.

 

 

Chanzo; Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: