Issa Faki kutoka Tanzania ameshinda pambano katika Mashindano ya Dunia ya Ngumi, na ushindi huu ni wa kwanza kwa Tanzania kwenye mashindano haya tangu mwaka 1974 miaka 51 iliyopita.
Katika siku ya tatu ya mashindano hayo huko Dubai, jumla ya mabondia 10 wa Afrika walifuzu kuingia hatua ya 16 Bora, na kufanya idadi ya mabondia wa Afrika kufika 18.
Ushindi wake ni wa kihistoria kwa sababu Tanzania haikuwa imeshinda pambano la Mashindano ya Dunia tangu Emmanuel Mlundwa mwaka 1974.
Ndiyo maana ushindi huu umeleta furaha kubwa sana kwa mashabiki wa ngumi nchini.
Mabondia 10 wa Afrika waliofuzu siku ya tatu
Issa Faki (Tanzania)
Amadu Mohammed (Ghana)
Ebener Ankrah (Ghana)
David Pina (Cape Verde)
Lenick Fernandes (Cape Verde)
Washington Wandera (Kenya)
Andrew Chilata (Zambia)
Mwengo Mwale (Zambia)
Haymanot Desalegn (Ethiopia)
Djibril Traore (Mali)
Wao wanajiunga na mabondia wengine 8 wa Afrika waliofuzu siku ya pili.
Tuzo za Mashindano
Dhahabu: $300,000
Fedha: $150,000
Shaba: $50,000
Robo fainali: $10,000
Umuhimu wa ushindi wa Issa Faki
Chanzo; Bongo 5