Klabu ya Al Ahly Cairo ya Misri inapambana kumsajili mshambuliaji wa Pyramids FC Fiston, Mayele katika dirisha dogo la mwezi January, mwakani.
Taarifa kutoka Misri zinadai Al Ahly wapo tayari kumlipa nyota huyo mshahara wa Paundi za Misri 3,476,902 (Sawa na Sh 180Mil) kwa mwezi.
Nyota ambaye ameibuka Mchezaji Bora kwa Vilabu vya Afrika katika msimu uliopita akiwa na msimu wake wa kwanza Pyramids akitokea Yanga ambayo ilimuuza msimu wa 2024/25.
Chanzo; Global Publishers