Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili salama Morocco kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) zinazotarajiwa kuanza Jumapili, Desemba 21.
Stars imewasili ikitokea Cairo, Misri ambako iliweka kambi ya maandalizi kwa takribani wiki mbili na kucheza mechi za kirafiki.
Taifa Stars iko Kundi C na itaanza kampeni yake Jumanne, Desemba 23 dhidi ya Nigeria ‘Super Eagles’, ikisaka matokeo chanya ya kihistoria katika michuano hiyo.
Ratiba ya mechi za Taifa Stars AFCON 2025 (Kundi C):
Desemba 23: Tanzania vs Nigeria
Desemba 27: Tanzania vs Uganda
Desemba 30: Tanzania vs Tunisia
Chanzo; Mwanaspoti