Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuahirishwa kwa hafla ya Tuzo za Msimu wa 2024/2025 ambayo awali ilipangwa kufanyika Desemba 5, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, uamuzi huo umetokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa waandaaji kwa kipindi hiki.
“Tarehe mpya ya kufanyika kwa hafla hiyo itatangazwa mara tu itakapopangwa,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
TFF imewahakikishia wadau na mashabiki wa soka kuwa watapewa taarifa mapema pindi maandalizi yatakapokamilika.
Chanzo; Global Publishers