Wasemaji wa klabu pinzani za jadi Simba SC na Young Africans SC Ahmed Ally na Ally Kamwe wameonekana pamoja leo wakiwa wamekaa meza moja katika tukio maalum lililotangaza mpango wa kukutanisha Mashabiki wa Timu hizo mbili katika Uwanja wa KMC tukio linalotarajiwa kuvuta hisia za Mashabiki wa soka nchini.
Akizungumza katika tukio hilo, Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally alisema maandalizi yanaendelea vizuri na lengo kuu ni kuandaa tukio lenye ushindani wa kirafiki, akisisitiza kuwa soka linapaswa kuwa chombo cha kuleta mshikamano na burudani kwa Mashabiki wa pande zote.
“Tumepanga tukio hili kwa lengo la kuwakutanisha Mashabiki wa Simba na Yanga katika mazingira ya amani na heshima, tukiamini litakuwa tukio la kipekee litakaloacha kumbukumbu nzuri,” alisema Ahmed Ally.
Chanzo; Millard Ayo