Bondia nguli wa Ndondi Duniani Mike Tyson, mwenye umri wa miaka 59, ametangaza rasmi kuwa pambano lake dhidi ya Bingwa wa zamani wa dunia, Floyd Mayweather Jr. litafanyika barani Afrika mwezi Machi 2026.
Ikimbukwe mwezi Septemba, Tyson alionyesha kushangaa kitendo cha mpinzani wake Mayweather kukubali kupambana naye, akisema “Hili ni jambo ambalo mimi hata dunia hatukutarajia lingeweza kutokea. bado siamini kwamba Floyd anataka kweli kupigana, hili litakuwa na athari kubwa kiafya kwake.”
Mayweather hakusita kujibu kupitia mitandao yake ya kijamii akindika “Nimekuwa nikifanya hili kwa miaka 30, na hakuna bondia hata mmoja aliyewahi kuharibu urithi wangu. Unajua kwamba kila ninachokifanya huwa ni kikubwa na cha kihistoria, Mimi ni bora zaidi kwenye biashara ya ndondi, hili pambano litawapa mashabiki kile wanachokitaka.”
Chanzo; Eatv