Kikosi cha Simba SC kimeondoka leo kuelekea nchini Tunisia kwa ajili ya mchezo muhimu wa CAF Champions League dhidi ya Espérance Sportive de Tunis.
Baada ya kuondoka, Kocha Mkuu wa Simba, Steve Robert Barker, alisisitiza kuwa kikosi kiko tayari kimwili na kiakili, huku akigusia usajili wa Clatous Chama akisema utaongeza ubora, uzoefu na ushindani ndani ya timu kuelekea michezo mikubwa ya kimataifa.
Simba inalenga kupata matokeo chanya ugenini, huku mashabiki wakihimizwa kuendelea kuisapoti timu yao kwa mshikamano na imani.
Chanzo; Global Publishers