Timu ya mpira wa kikapu ya Dar City imechukua tena ubingwa wa Ligi ya NBL baada ya kuibuka na ushindi wa vikapu 80–51 dhidi ya timu ya Kisasa HRS, katika mchezo uliofanyika jijini Dodoma. Baada ya mchezo huo, timu hiyo ilikabidhiwa kombe na Waziri wa Madini (Mbunge) Antony Mavunde.
Dar City imeendelea kuwa tishio ndani na nje ya Tanzania, ikiwa ni takribani mwezi mmoja tangu itwaa ubingwa wa Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam na kufanikiwa kuvuka hatua ya kuingia BAL 2026, baada ya kushinda michezo mitatu kwenye mashindano ya Road to BAL yaliyofanyika jijini Nairobi, wiki mbili zilizopita.
Chanzo; Global Publishers