Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Man United Yamkana Ramos

Manchester United imepotezea mpango wa kumsajili beki mkongwe wa Real Madrid, Sergio Ramos, katika dirisha dogo la Januari 2026.

Man United ilianza kuhusishwa na taarifa za kumsajili Ramos baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 kuwa huru, kufuatia kuondoka Monterrey ya Mexico mwanzoni mwa mwezi huu.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa za ESPN, Manchester United imekanusha taarifa hizo kwa kusema haina mpango wowote wa kumsajili Ramos na haitafuatilia dili hilo, ambalo tayari limeshaanza kuibua hisia tofauti kutoka kwa mashabiki wake.

Ramos, anayejivunia mafanikio makubwa kwenye soka, amewahi kushinda Kombe la Dunia 2010, Kombe la Ulaya (UEFA Euro) mara mbili, mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na mataji matano ya La Liga.

Hata Hivyo Man United imesisitiza itafanya usajili wa baadhi ya wachezaji Januari 2026, ili kuboresha kikosi chao, kufuatia mapendekezo ya kocha Ruben Amorim.

 

 

Chanzo; Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: