Shirikisho la soka la kimataifa (FIFA) imependekeza matumizi ya VAR kwa mipira ya kona wakati wa fainali za Kombe la Dunia 2026, ili kuepuka makosa yanayoweza kujitokeza na kuibua sintofahamu kwa wachezaji, makocha na mashabiki.
FIFA inataka kuruhusiwa kutumia VAR katika maamuzi ya mipira ya kona katika Kombe la Dunia ili kuepuka makosa yanayoweza kumsababisha aibu, hususan katika mechi za fainali.
Pendekezo la kutumia VAR kusahihisha mipira iliyotolewa vibaya limewahi kupungwa baada ya kupendekezwa na jopo la kiufundi la wanasheria wa soka mwezi uliopita. Hata hivyo, Bodi ya Kimataifa ya Sheria za Mpira wa Miguu (IFAB), inayounda sheria za mchezo, inaweza ikaruhusu matumizi ya VAR kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 na mashindano mengine.
Hali hii inaweza kuibua mjadala ndani ya Ligi Kuu ya EPL, kwani kocha wa Nottingham Forest, Sean Dyche, hivi karibuni alilalamika kuhusu ukosefu wa uhakiki wa VAR baada ya kufungwa kwa mabao kutokana na mipira iliyotolewa vibaya ya kona katika michezo mfululizo.
FIFA inataka kuwa na zana zaidi ili kuepuka makosa yanayoweza kusababisha aibu, hususan katika mechi za fainali za Kombe la Dunia 2026. Taarifa zinaonyesha kwamba, FIFA ndicho chombo kilichopendekeza kwa mara ya kwanza kutumia VAR kusahihisha maamuzi yasiyo sahihi ya mipira ya kona.
Chanzo; Mwanaspoti