Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, ametoa taarifa ya wachezaji majeruhi kuelekea mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Wolves.
Arteta amesema beki wa Ufaransa William Saliba anakaribia kurejea uwanjani baada ya kukosekana tangu Novemba 26.
Hata hivyo kocha huyo raia wa Hispania amesema, ataangalia mazoezi ya leo ili kuthibitisha kama beki huyo atacheza katika mechi ya kesho Jumamosi, Desemba, 13, 2025.
“Kama ni mechi dhidi ya Everton wiki ijayo, naamini atakuwa fiti. Kwa kesho bado hatujui.”
Kuhusu wachezaji wengine kama Jurrien Timber, Declan Rice na Leandro Trossard, Arteta hajathibitisha kama watakuwa tayari baada ya kukosa mechi dhidi ya Club Brugge.
Mashabiki wa Arsenal wanatarajia kwa hamu kuona nani atarejea kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Arteta katika mechi zijazo.
Chanzo; Mwanaspoti