Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah, ameashiria kuwa huenda mchezo wa dhidi ya Brighton ukawa mechi yake ya mwisho kabisa katika uwanja wa Anfield.
Akizungumza na ViaPlay, Salah alisema:
“Niliwapigia mama na wazazi wangu nikawaambia… njoo kwenye mechi dhidi ya Brighton. Sijui kama nitacheza au la, lakini nitaifurahia kwa hali yoyote.”
Salah pia aliongeza kuwa ana mpango wa kuwapo Anfield kuwaaga mashabiki kabla ya kujiunga na Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON)
“Nitakuwa Anfield kuwaaga mashabiki… kisha niende kwenye Kombe la Afrika. Sijui nini kitatokea nikiwa huko, sijui nini kitaendelea baadaye.”
Akitamka hisia zake za kudumu kwa klabu hiyo, Salah alisema
“Nitaiipenda na kuisapoti Liverpool daima. Mimi na watoto wangu… Liverpool itakuwa milele timu yangu.”
Chanzo; Bongo 5