Stephane Aziz Ki ameondoka Wydad AC ya Morocco na kujiunga na Al Ittihad ya Libya kwa mkataba wa miaka miwili.
Usajili wa nyota wa zamani wa Sevilla na timu ya Taifa ya Ufaransa, Wissam Ben Yedder ambao Wydad AC itaukamilisha hivi karibuni, unaonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa kuishawishi klabu hiyo kumfungulia mlango wa kutokea Aziz Ki.
Al Ittihad imelipa kitita cha Dola 300,000 (Sh 825 milioni) ili kuipata saini ya kiungo huyo wa timu ya taifa ya Burkina Faso.
Chazo; Eatv