Klabu ya Simba SC imetangaza rasmi kuachana na kocha Dimitar Pantev, kutokana na matokeo yasiyoridhisha na changamoto zilizojitokeza katika michezo ya hivi karibuni.
Uamuzi huo umetokea ghafla, na umewashangaza mashabiki wengi wa timu hiyo.
Baada ya kuondolewa kwa Pantev, Matola amepewa jukumu la kukiongoza kikosi cha Simba kwa muda, katika kipindi hiki muhimu kuelekea mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City itakayochezwa keshokutwa Alhamisi, kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, jijini Dar es salaam.
Chanzo; Mwanaspoti