Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Hilda Atundika Rekodi kwa Kupika Pilau 8,750

pishi wa Nigeria, Hilda Baci ameshinda tuzo akiweka rekodi yake ya tatu ya Guinness World Records (GWR) baada ya kuandaa mchele na kupika pilau kilo 8,780 mchele kwa wakati mmoja.

Taarifa ya kuweka rekodi hiyo mpya imetangazwa Jumanne Januari 20, 2026 na Mkuu wa Ushirikiano wa Wateja wa Guinness World Records, Andrew Fanning, ambapo wamempongeza Baci kwa kutambuliwa akiweka rekodi ya ziada, ikieleza kuwa mafanikio hayo yamekidhi vigezo vya kuweka rekodi ya dunia.

Rekodi hiyo ya mapishi ya pilau kilo nyingi zaidi kwa wakati mmoja, imemuongezea sifa ya kuandaa sufuria kubwa zaidi ya wali wa jollof katika mtindo wa mapishi ya Nigeria.

Rekodi hiyo ya kupika kilo nyingi za mchele iliwekwa Septemba 12, 2025 Victoria Island, Lagos nchini Nigeria, ambapo Baci kwa kushirikiana na chapa ya chakula Gino waliandaa jumla ya kilo 8,780 za mchele.

Awali, wakati akiandaa tukio hilo, ililenga kuvunja rekodi ya wali wa jollof, lakini Guinness baadaye ilithibitishwa kuwa jaribio hilohilo pia lilistahili kuchukuliwa kama sufuria kubwa zaidi la kupikia.

Kwa mujibu wa Guinness World Records, maelezo rasmi ya rekodi hiyo ni kama ifuatavyo:“Sufuria kubwa zaidi la wali lina uzito wa kilo 8,780 na ilipatikana kutoka kwa Hilda Baci na Kampuni ya Gino Septemba 12, 2025.”

Ikumbukwe Hilda alipata umaarufu mwaka wa 2023 baada ya kuvunja rekodi na kuingia katika kitabu cha rekodi ya dunia cha ‘Guinness World Record’ (GWR) kwa kupika masaa 100 bila kupumzika lakini rekodi hiyo ilivunjwa na Alan Fisher ambaye alipika siku nane sawa na saa 199.

 

 

Chanzo;  Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: