Bondia mkongwe kutoka Marekani, Mike Tyson, ameibua mjadala mtandaoni baada ya kufichua kwamba familia yake iliogopa alipoamua kuacha kwa muda mfupi kuvuta bangi. Tyson amesema familia ilimuomba aendelee kuvuta, kwa sababu waliona mabadiliko yasiyo ya kawaida.
kwenye podcast ya Confidence of Champions, Tyson alielezea jinsi kuacha bangi kwa siku tano tu kulivyomfanya ajisikie kama mtu tofauti kabisa na alivyozoeleka.
"Mke wangu na watoto wangu waliogopa, walikuwa wakisema tafadhali vuta baba tafadhali kwa sababu kwa kipindi chote nilikuwa mkali sana" amesema Mike.
“Watu wanaoishi karibu nami, wakinitazama tu, wanasema ‘Wow’. Nimekuwa mtu wa tofauti kabisa.”
Aidha aliongezea kwa kueleza “Ninapokunywa pombe, inamfanya kuwa kama mpumbavu lakini nikivuta bangi na kuwa mtulivu na hufikiria. Ni bora kuliko kunywa na kuwa mshenzi.”
Chanzo; Mwananchi Scoop