Tanzania, Kenya na Uganda rasmi zimekabidhiwa uenyeji wa AFCON 2027 baada ya mechi ya fainali kati ya Senegal vs Morocco ambapo Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda.
Makonda ameungana na viongozi wengine wa Michezo Afrika Mashariki kupokea bendera ya CAF waliyokabidhiwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu Afrika, Patrice Motsepe kama ishara sasa rasmi kupokea kijiti cha uenyeji kutoka kwa Morocco.
Chanzo; Millard Ayo