Mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappé, ameweka rekodi ya kipekee katika ulimwengu wa soka baada ya kuwa mchezaji wa nne duniani katika karne ya 21 kufunga magoli 60 au zaidi ndani ya mwaka mmoja kwa upande wa klabu na timu ya taifa.
Hatua hiyo inamuweka mshambuliaji huyo wa Real Madrid kwenye orodha ya wachezaji wachache sana waliowahi kufikisha idadi ya mabao 60 au zaidi, orodha ambayo awali iliwahusisha magwiji kama Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Robert Lewandowski.
Mbappé amefikia mafanikio hayo makubwa huku bado akiwa na mechi kadhaa zilizobaki kabla ya kufikia Januari Mosi 2026, jambo linaloongeza uwezekano wa kuifanya rekodi yake kuwa kubwa zaidi.
Lionel Messi - mabao 91 (2012)
Cristiano Ronaldo - mabao 60 (2011)
Cristiano Ronaldo - mabao 63 (2013)
Robert Lewandowski - mabao 69 (2021)
Chanzo; Eatv