Mwanamieleka nguli wa WWE, John Cena ametangaza kustaafu rasmi mchezo huo baada ya kumalizika kwa mchezo wake wa mwisho usiku wa kuamkia leo.
Siku chache zilizopita, nyota huyo wa WWE alitangaza uamuzi wake wa kustaafu rasmi mchezo wa mieleka baada ya kuutumikia kwa takribani miaka 25.
Uamuzi huo uliwashangaza na kuwahuzunisha mashabiki wengi, ambapo wengi wao walionesha kutofurahishwa na hatua hiyo, wakisema bado walitamani kumuona akiendelea kupambana ulingoni.
Chanzo; Global Publishers