Klabu ya Kinondoni MC FC imethibitisha kusitisha mkataba na Kocha Márcio Máximo pamoja na benchi lake la ufundi huku ikieleza kutambua na kuthamini jitihada walizofanya katika kuboresha utendaji wa timu, ndani na nje ya uwanja, kwa ngazi ya mchezaji mmoja mmoja na timu kwa ujumla.
“Hata hivyo, mabadiliko hayo hayakuweza kuleta matokeo ya haraka, kwani yanahitaji muda wa kutosha ili kuzaa matokeo yanayotarajiwa.” imesema taarifa rasmi iliyotolewa KMC FC leo Desemba 6, 2025.
“Tunamtakia Kocha Maximo na timu yake kila la heri, na tunabaki wazi kuwatumia tena pindi fursa itakapojitokeza siku za usoni.” imesema taarifa hiyo.
Chanzo; Nipashe