Pendekezo jipya kutoka kwa serikali ya Donald Trump linawataka wageni wanaopanga kwenda Marekani kufichua shughuli zao kwenye mitandao ya kijamii katika kipindi cha miaka mitano kama mojawapo ya masharti ya kuingia nchini humo.
Taarifa hizo zimetolewa jana Alhamisi, miezi sita kamili kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la FIFA la 2026, ambalo Marekani itaanda kwa kushirikiana na Mexico na Canada.
Hata hivyo bado haijafahamika wazi namna ukaguzi wa taarifa za mitandao ya kijamii za watu hao itakavyofanyika.
Shirikisho la soka duniani FIFA halijatoa maoni yoyote hadi sasa kuhusu pendekezo hilo la Marekani.
Michuano ya Kombe la Dunia inatarajiwa kuvutia maelfu ya mashabiki kutoka kila pembe ya dunia watakaohudhuria mechi mbalimbali katika viwanja 16 vitakavyotumika.
Chanzo; Dw