Ziara ya Lionel Messi nchini India ilianza kwa vurugu jana Jumamosi, Desemba 13 baada ya mashabiki kung’oa viti na kuvitupa sehemu ya kuchezea, kufuatia ziara fupi ya mshambuliaji huyo wa Argentina na klabu ya Inter Miami katika Uwanja wa Salt Lake, Kolkata.

Maelfu ya mashabiki walifurika uwanjani kwa ajili ya kumwona Messi, lakini ulinzi mkali na upatikanaji mdogo kumuona uliwafanya mashabiki wengi wakisubiri kwa saa kadhaa bila mafanikio.
Baadhi ya mashabiki walikasirika, wakavunja vizuizi na kuingia uwanjani baada ya Messi kuondoka mapema kuliko ilivyotarajiwa.
Chanzo; Mwanaspoti