Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, Gianni Infantion amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ambapo wamejadiliana kuhusu miundombinu na jinsi FIFA na Tanzania wanavyoweza kushirikiana kutoa fursa kwa Vijana.
Baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika Morocco, Rais wa FIFA ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram akisema “Ilikuwa vizuri kukutana na ujumbe kutoka Tanzania kujadili maendeleo ya miundombinu ya soka na jinsi tunavyoweza kushirikiana ili kutumia vema miradi mbalimbali ya FIFA ili kusaidia kuunda njia na kutoa fursa kwa Vijana kupitia mchezo wetu huu mzuri”
“Tulizungumzia umuhimu wa maendeleo ya ngazi za chini, tukigusa mradi wa FIFA Arena na Mpango wa Maendeleo ya Vipaji wa FIFA”
“Asante kubwa kwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, Katibu Mkuu wake Gerson Msigwa, Neema Msitha na Balozi Ali Mwadini kwa muda wenu na kuwa tayari kufanya kazi panoja kumsaidia kila Mtanzania kupitia ndoto kupitia ya soka”
Chanzo; Millard Ayo