Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Ronaldo Afungua Night Club, Simu Marufuku

Nyota wa soka duniani, Cristiano Ronaldo, ameendelea kuvutia vichwa vya habari baada ya kuingia katika biashara ya burudani kwa kufungua klabu ya kifahari jijini Madrid, Hispania, yenye amri ya kutotumia simu za mkononi ndani.

Klabu hiyo inalenga watu mashuhuri, wafanyabiashara na watu wenye ushawishi wanaotafuta mazingira ya faragha kwa ajili ya kujidai bila usumbufu. Uamuzi wa kupiga marufuku simu unaelezwa kuwa ni kwa ajili ya kutunza faragha za watu.

Ndani ya klabu hiyo kunatajwa kuwepo maeneo ya mikutano, sehemu za kupumzika, migahawa ya kifahari, pamoja na nafasi za kujenga mitandao ya kibiashara (networking). Wageni watalazimika kuacha simu zao nje au kuzihifadhi sehemu maalum kabla ya kuingia.

Hatua ya Ronaldo imepokelewa kwa hisia tofauti, huku wengine wakiona ni wazo bunifu linaloendana na mahitaji ya sasa ya faragha, na wengine wakijiuliza kama itawezekana kuishi bila simu hata kwa muda mfupi.

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: