Mwanaume raia wa Afrika Kusini, anayetajwa kuwa mvutaji sigara mkongwe zaidi duniani, Jan Steenberg, amefariki dunia Januari 6, 2026 chache baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Kwa mujibu wa taarifa, Steenberg alidai kuwa na umri wa miaka 121, na katika mahojiano yake aliwahi kusema alianza kuvuta sigara akiwa na umri wa miaka 14. Inaripotiwa kuwa alifariki dunia kutokana na shambulio la pumu (asthma attack) wiki chache zilizopita.
Kifo chake kimewaacha wengi wakiwa na mshangao mkubwa, hasa kutokana na madai ya umri wake mkubwa na historia ndefu ya uvutaji sigara. Familia, marafiki na wananchi wameendelea kutoa salamu za rambirambi wakimuombea apumzike kwa amani.
Chanzo; Global Publishers