Mwanamuziki maarufu wa reggae kutoka Jamaica, Jimmy Cliff, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81, taarifa imethibitishwa na mke wake, Latifa Chambers.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Latifa alieleza kuwa msanii huyo amefariki kutokana na ugonjwa wa kuanguka (fall illness) na nimonia, akikumbusha dunia ukubwa wa kipaji cha gwiji huyo ambaye aliiacha reggae ikiwa na alama isiyofutika.
Katika maisha yake ya sanaa, Jimmy Cliff alitamba na vibao vilivyotikisa duniani kama “You Can Get It If You Really Want,” “I Can See Clearly Now,” na “Wonderful World,” ambavyo vilimpa hadhi ya kuwa miongoni mwa wanamuziki wenye mchango mkubwa katika historia ya reggae.
Chanzo; Global Publishers