Madame President Frida Amani, ameendelea kuvunja rekodi zake mwenyewe, mwaka jana alipata nafasi ya ku-perform mbele ya Marais 15 na mwaka huu mbele ya viongozi wa nchi zaidi 170,
UNEA 7 ni mkutano unaowakutanisha viongozi wa nchi mbalimbali kuweza kujadili namna ya kuweza kuyatunza mazingira, ambapo mwaka huu walilenga zaidi katika kujadili suluhisho endelevu kwa sayari yenye ustahimilivu.
Ni heshima ya kipekee kama nchi kuweza kupata nafasi kwani Frida Amani, ndio mwanahiphop wa kwanza Duniani kuweza kutumbuiza kwenye jukwaa hili,
Nafasi hii inakuja mara tu alipotangzwa kuwa balozi na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira (UNEP) kuwa mchechemuzi wa urejeshwaji wa mifumo ya ikolojia.
Chanzo; Clouds Media