Muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Miriam Chirwa, ameonyesha furaha na shukrani kubwa kwa Mungu baada ya kupata mchumba.
Akizungumza na Global TV, Miriam amesema kuwa ni neema ya kipekee kwa Mungu kumwongoza hadi kumpata mtu wa kumpenda na kumheshimu. Ameeleza kuwa anashukuru kwa safari yote aliyopitia na jinsi Mungu alivyomjalia katika kipindi hiki maalum cha maisha yake.
Aidha, Miriam amesisitiza kuwa kwa sasa hana mengi ya kusema zaidi ya kumshukuru Mungu kwa wema na baraka alizopewa. Amesema anajisikia furaha na amani moyoni, na kwamba kila hatua anayochukua inaongozwa na Mungu.
Chanzo; Global Publisers