Mama wa rapa na Sean “Diddy” Combs, Janice Combs, amekanusha madai yaliyoibuka kwenye documentary ya Netflix Sean Combs: The Reckoning, iliyotolewa Desemba 2, 2025.
Kwenye tamko lake, Janice alisema taarifa kuhusu malezi na maisha ya familia yake zimepotoshwa kwa makusudi. Amesisitiza kuwa hakuwahi kuwa mzazi mkatili, aliyelea Diddy kwa upendo, bidii, na kujitolea, na amekanusha madai kwamba mwanawe alimwagi kofi.
Janice pia alibainisha kuwa baadhi ya watu wanatumia matukio ya huzuni ya kihistoria kwa maslahi yao binafsi, jambo aliloliona la kusikitisha na lisilokubalika. Kauli yake imeibua mjadala mtandaoni kuhusu mipaka ya documentaries katika kusimulia hadithi za watu mashuhuri.
Chanzo; Bongo 5