Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayewakilisha lebo ya Wasafi, Zuchu amepokea pongezi nyingi kutoka kwa mashabiki wakisifia uwezo wake wa kubadilisha namna ya uimbaji kwenye kila wimbo anaotoa.
Zuchu ambaye ameachia wimbo wake mpya wa Reason Novemba 22, 2025, ambao upo kwenye mtindo wa rege ukiwa kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa kwa mashabiki zake, ameendelea kufanya aaminike zaidi katika kuuchezea muziki anavyotaka
Hatahivyo, kati ya nyimbo tatu alizoachia Zuchu baada ya albamu yake ya Peace and Money zimekuwa na utofauti zikipishana aina na namna ya uimbaji wake, hali inayotafsiriwa na mashabiki kuwa msanii huyo anabadilika zaidi.
Baada ya Albamu ya Peace And Money iliyotoka Desemba 20, 2024, Zuchu aliachia nyimbo zingine tatu ambazo ni Amanda ambayo ni Afro Pop iliyochanganyikana na Bongo Fleva, Inama ft Diamond Platnumz ambayo ni Bongo Fleva na Reason ambayo ni Rege. nyimbo hizo tatu zinakuwa kazi pekee kwa msanii huyo kuachia mpaka kufikia Novemba 22, 2025.
Chanzo; Mwananchi Scoop