Muigizaji Cary-Hiroyuki Tagawa amefariki, Desemba 4, 2025, akiwa na umri wa miaka 75. Sababu ya kifo chake ni matatizo kutokana na mshtuko wa damu (stroke au cerebrovascular accident - CVA). Alifariki Santa Barbara, California, mtoto wake Penny Zizcarra amethibitisha.
Tagawa alikuwa mwigizaji maarufu kimataifa, hasa kwa kuigiza Shang Tsung katika filamu na michezo ya Mortal Kombat, pamoja na majukumu mengine katika filamu kama The Last Emperor, Memoirs of a Geisha, na vipindi vya TV kama The Man in the High Castle na Nash Bridges. Alishiriki katika zaidi ya 150 matoleo ya filamu, TV na michezo ya video kwa zaidi ya miaka 40 ya kazi yake.
Chanzo: Tanzania Journal