Msanii Wa Nigeria, African Giant Burna Boy ameweka rekodi mpya baada ya kufikisha zaidi ya watu milioni 100 waliotafuta kazi zake kupitia Shazam, na hivyo kuwa msanii wa pili (2) kutoka Afrika kufanikiwa kufikia hatua hiyo. Huku Wa Kwanza Akiwa Ni Big Wiz,
Shazam, ambayo ni programu inayotumiwa na watu duniani kote kutambua nyimbo, imekuwa kipimo muhimu cha umaarufu wa muziki kimataifa. Kiwango hiki cha mafanikio kinaonyesha ukubwa wa ushawishi wa Burna Boy katika tasnia ya muziki duniani, hasa kupitia nyimbo maarufu kama Ye, Last Last Na Zingine Kibao.
Chanzo; Wasafi